Delray Is In Moshi's Swahili Newspaper:

Jiji la Delray Beach laipiga jeki Maktaba

Na Daniel Mjema, Moshi

Jiji la Delray Beach la Florida nchini Marekano ambalo lina uhusiano dada na mji wa Moshi limetoa msaada wa  kompyuta tano na gharama za kuunganishia Interneti kwa maktaba ya mkoa wa Kilimanjaro.

            Uzinduzi wa huduma hiyo ya mawasiliano ilizinduliwa juzi katika maktaba hiyo na ujumbe wa wa Wamarekani, ukiongozwa na Mwenyekieti wa ushirikiano wa miji hiyo, Ngozi Mensah na mkewe.

            Kompyuta hizo tano mpya zina thamani ya Sh 5 Milioni ambapo Jiji la Delray Beach limetoa Dola 720 za Marekani kulipia huduma ya Interneti kwa mwaka mzima na pia dola 360 za kuunganishiwa huduma hiyo.

            Katika ujumbe huo unaomjumuisha Mearekani n’Detenga n’Gurumo, Mensah alitumia fursa hiyo kusoma salamu za Meya wa Jili la Delray Beach, Rita Ellis ambaye alisema Wamarekani wanafurahishwa na mahusiano hayo.

            Ellis katika salamu zake hizo amefafanua kuwa lengo hasa la Jiji lake ni kuhakikisha kunaanzishwa mpango wa kubadilishana walimu, wanafunzi na Biashara kati ya Jiji hilo na Mji wa Moshi.

            Katika taarifa yake, Mkutubi wa Maktaba ya mkoa wa Kilimanjaro, Mariam Mndeme alisema tangu waanze kunufaika na misaada kutoka Marekani, Idadi ya wasomaji imeongezeka kutoka 1,338 mwaka 2001 hadi 3,047.

            Mndeme alitaja misaada ambayo Maktaba hiyo imenufaika nayo ni pamoja na msaada wa dola 15,000 uliotlewa kwa ajili ya kukarabati Jengo la maktaba, vitabu 20,000, kompyuta tano zilizokwishatumika zilizotolewa 2002.

            Katika kipindi hicho, Maktaba hiyo ilipokea msaada wa vitabu vipya 458 kwa ajili ya watoto ambavyo vimesaidia kuinua kiwango chao cha taaluma.

            Mkutubi huyo alisema maktaba yake inakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwamo udogo wa Jengo na kuchakaa kwa samani ambazo zilinunuliwa miaka 37 iliyopita.

----------------------

The English transltion by Ndehoria Ndesamburu is printed below:

''DELRAY BEACH CITY HAS DONATED TO MOSHI LIBRARY''
 
The city of Delray Beach in Florida, America which is a sister city of Moshi has donated 5 computers and the costs of internet connection to the library in Kilimanjaro Region.
 
The opening of that services of communication was opened a day before in that library with a message from Americans, led by chairperson of the co-operation of the two cities, Ngozi Mensah and his wife.
 
The five computers worth TShs. 5.0 Million.  Delray Beach paid US $780 for internet connection for one year and $360 as connection fee for that service.
 
In that message where by Mr. n'Detenga n'Gurumo is included, Mr. Mensah used the opportunity to read greetings from Mayor of Delray Beach, Ms. Rita Ellis whereby she said Americans are happy with the relationship between the two cities. On the greetings from Ellis, she has explained that the main purpose for her city is to make sure they start a program of exchanging teachers, students and business for both two cities.
 
From the report of the Librarian of Moshi Municipal Public Library, Ms. Miriam Mndeme has indicated that since they started to enjoy the donations from America, the number of people using the library has increased from 1338 in the year 2001 to 3047 at present.
 
Ms. Mndeme mentioned some of the donation which the library has benefited includes cash US $15,000.00 for renovation of the building, books $20,000.00, and 5 used computers which were donated in 2002.
 
During that period, the library has received 458 new books for children which have helped to raise their level academically.
 
The librarian said that, this library is suffering from different problems such as being a small library building and the wear and tear of furniture which were bought 37 years ago''.